KUHUSU SISI

KUHUSU SISI– DEVELOPERS GROUP NI jumuiya ya wanafunzi na wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) iliyoundwa kwa lengo la kujifunza, kushirikiana maarifa, na kuhamasisha ubunifu katika sekta ya teknolojia. Tunaunda mazingira rafiki na ya msaada ambapo kila mwanachama ana nafasi ya kukuza ujuzi wake kupitia mijadala, mafunzo ya vitendo, miradi ya pamoja, na ushauri wa kitaalamu. MALENGO YETU Kukuza uelewa wa teknolojia miongoni mwa wanachama. Kutoa majukwaa ya kujifunza kupitia kozi, semina, na warsha. Kuwezesha ushirikiano wa miradi ya kiteknolojia. Kuandaa fursa za maendeleo ya kitaaluma na ubunifu. Tunachofanya : Mafunzo ya Programu na Mitandao. Ushirikiano kwenye miradi ya Tech & Innovation. Kushiriki mashindano ya ICT. Kutoa msaada wa kitaalamu kwa wanafunzi na jamii. Jiunge nasi na kuwa sehemu ya mabadiliko ya kidigitali. Karibu DEVELOPER GROUP– Ma...